Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MKUU  wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amezitaka Taasisi mbalimbali  za Dini kujitolea katika kuchangia madawati ili iweze kukabilina na changamoto za madawati katika wilaya hiyo.

Hapi, ameseyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokabidhiwa hundi ya sh. Milioni 19 kutoka kwenye kanisa la The Pool of Siloam Church kwa ajili ya kusaidia kumaliza tatizo la madawati.

Amesema kitendo cha Kanisa hilo kusaidia tatizo la madawati ni jambo jema ambalo litasaidia kumalizana na changamoto ya madawati huku akitaka taasisi zengine kuiga mfano wa kanisa hilo.

Amesema kwa sasa Wilaya yake inakalibia kumaliza changamoto ya ukosekanaji wa madawati ambapo amedai mpaka kufikia mwisho wa mwezi uwenda tatizo la madawati akatika wilaya hiyo litakuwa limekamilika.

Hata hivyo, Hapi amewataka watendaji wa manispaa hiyo kuhakikisha wanazipeleka pesa hizo zilizotolewa kunakohusika na sio sehemu nyingine.

Aliongeza kuwa yeye yuko tayari kuwafuata viongozi wa dini ili waweze kumsaidia katika kampeni ya madawati katika kumaliza tatizo hilo katika halmashauri ya Kinondoni kwa wanafunzi kuachana na kukaa chini ya sakafu.

Amesema kanisa kujitoa huko atafikisha salamu kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutokana na mwitikio wa kutambua umuhimu wa elimu na kukubali kuchangia.

Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya  amesema kuwa mchango wa fedha hizo kwa ajili ya madawati imetokana na mchango wa waumini wa kanisa hilo kwa kuguswa na madawati.

Eliya amesema ataendelea kuchangia katika hatua mbalimbali kutokana nafasi ya kanisa katika jamii hasa katika matatizo mbalimbali.
 Mkuu wa Wilaya, Ally Hapi akizungumza  na waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church ambao wamefika katika viwanja vya manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kumkabidhi hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Jacob  Boniface.
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akitoa neno la shukrani katika hafla ya kumkabidhi  hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
 Wakili wa Mungu wa Kanisa la The Pool of Siloam Church, Elisha Eliya akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waumini wa kanisa la The Pool of Siloam Church waliofika kushuhudia makabidhiani ya mfano wa hundi ya sh.milioni 19 ya  kutengeneza madawati kwa shule za msingi na sekondari za manispaa ya kinondoni, leo jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2016

    nafikiri ingekuwa vizuri kubuni vyanzo vingine vya kuchangia suala hili au masuala mengine kama haya maana suala hili likiingia kwenye makanisa wanaoumia ni watu wenye kipato kidogo. mtu akiambiwa atoe mchango kanisani yuko radhi kutoa hata akiba ndogo aliyonayo maana usipotoa kanisani na ndio jumuia yako mtu anaogopa akipata shida labda hatasaidiwa.pia usipotoa kanisani basi wewe humtolei Mungu. makanisa na sehemu za kuabudia zibaki kuwa sehemu za kuabudia,kukua kiroho na sio sehemu ya kuwa na hofu kuwa sijachanga mchango wa madawati,visima,ujenzi wa hospitali. Yajiimarishe kivyake ila yasiingie katika mambo ya serikali maana hapa itakuja tokea watu wachache wanaotaka kukuza majina yao watawaumiza wenzao na kutumia neno la Mungu visivyo.Mtu ambaye roho yake inamtuma kuchangia basi apeleke mchango wake binafsi kwa mkuu wa wilaya au kunakohusika.Hebu tulitafakari hili kwa undani jamani tusije tukahukumiwa huko mbele.Ni maoni yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...