Katika mizunguko ya hapa na pale ndani ya Jiji la Mbeya, kamera ya Globu ya Jamii iliweza kuzinasa Taswira za wafanyabiashara ndogo ndogo katika soko mjinga eneo la Ilemi Darajani wakifanya biashara zao katika mazingira ambayo sio rafiki kabisa kwao na hata kwa wanunuzi wa bidhaa zinazouzwa katika soko hilo, kwani kando ya soko hilo kuna kihifadhi taka (dampo la taka) ambacho kimejaa sana na kupelekea uchafu kuzagaa ovyo eneo lote hilo, jambo linaloweza kuhatarisha afya ya muuzaji na hata mnunuzi pia. Inadaiwa kuwa ni muda mrefu sasa umepita bila kuonekana kwa wahusika wa kubeba taka katika eneo hilo, na hiki ni Kijipu Upele kinachosubiria kutumbuliwa katika eneo hili, hivyo shime shime wahusika kulifanyia ufumbuzi jambo hili.
Biashara zikiendelea eneo la Ilemi darajani waliopo kabara na kiweka taka chenye kumeremeta nyuma ya ofisi zao.
Wahusika wazoe taka ili kuto athiri afya za wafanya biashara hawa na walaji waa bidhaa hizi.
ReplyDelete