Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza SHIUMA, ulilenga kujadiliana na wadau wengine wa Uwekezaji ikiwemo taasisi za kifedha, juu ya Kurasimisha biashara zao na kuwekwa kwenye mifumo rasmi ya Kibiashara na Kijamii.
Machinga wamesema changamoto kubwa zinazowakabiri ni Ukosefu wa Mitaji ya Biashara, Maeneo ya Kufanyia Biashara pamoja na Ukosefu wa Elimu Biashara. Wamesema wanataka nao watambulike na taasisi za kifedha ili wapate fursa ya kukopesheka ili kukuza mitaji yao.
Katibu wa Shirika la Machinga Mkoa wa Mweanza SHIUMA, Venatus Anatory, akizungumza katika Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...