Na Abdulaziz Video,Lindi
Madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa na Ruangwa Mkoani Lindi Zimeanza Utekelezaji wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) kwa Kupatiwa Mafunzo ya Siku 4 na Kuratibiwa na Tamisemi
Kuanza kwa Hatua Hiyo kunafuatia kumalizika kwa Mafunzo kwa Watendaji wa Halmshauri 6 Za Mkoa wa Lindi juu ya Namna ya Kushiriki na Kutekeleza Mradi huo Utakaotekelezwa kwa Kipindi cha Miaka 5 Ijayo
Akifungua Mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amezitaka Halmashauri Hizo Kufuatilia kwa Umakini Mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo ili Kupata Uelewa Juu ya Uendeshaji wa Halmashauri
‘’ Madiwani ni kiungo muhimu baina ya serikali na watendaji wa serikali madiwani Musipokuwa Vizuri Mtaburuzwa na Watendaji hususan katika Utendaji na Utekelezaji wa Miradi hasa Ikiwa Diwani Una Tabia ya Kuomba omba na Kukopa kwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara Lazima Mjipime Nyie Ndio wamiliki wa Halmashauri au hamjijui?’’Alimalizia Zambi

Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Akitoa Hotuba yake ya Ufunguzi ambapo Pia Aliwataka
Madiwani Kuacha Siasa katika Kutekeleza Maendeleo ya Halmashauri
zao,Kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa Mradi wa Ps,Bw Conrad Mbuya

Madiwani wa Ruangwa Pamoja Na Mwandishi wa Vikao Vya Baraza la Madiwani Ruangwa,Bahati kasabano (Kulia)wakifuatilia mafunzo hayo

Afisa
Mshauri wa Masuala ya Utawala Bora PS3, Nazar Sola akitoa Elimu kwa
Madiwani juu ya Utekelezaji wa Mifumo ya Utendaji na Utoaji Huduma

Baadhi
ya madiwani na watendaji wa halmashauri za Kilwa na Ruangwa Mkoani
Lindi wakifuatilia jambo katika semina Elekezi ya Kujenga Uelewa kwa
Halmashauri kupitia Mradi kuimarisha Uwezo wa Kutoa Huduma kwa Jamii
Chini ya Utekelezaji wa Mradi wa PS3 Unaofadhiliwa na USAID.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...