Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameiomba serikali ya MALAYSIA kujenga ofisi za ubalozi wake hapa
nchini ili kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo leo Juni 24, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA ambaye
aliongozana na Balozi wa MALAYSIA aliye na makazi yake jijini Nairobi Kenya, ISMAIL SALAM walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini Dar Salaam.

Makamu wa Rais amesema ujenzi wa ofisi za ubalozi huo hapa nchini utarahisisha kwa kiasi kikubwa Watanzania wanaotaka kusafiri kwenda nchini MALAYASIA kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za masomo na biashara kuliko hali ilivyo sasa ambapo ofisi za balozi hizo zipo Nairobi – Nchini KENYA.

Kwa upande wake Waziri asiye na Wizara Maalum Dkt SRI IDRIS JALA amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi yake itaendelea kuimarisha,kukuza na kuendeleza mahusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia hasa uanzishaji wa ubalozi wake hapa nchini.

Hata hivyo, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa Makubaliano ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malaysia ambayo yatajikita katika sekta mbalimbali zikiwemo za elimu, uchukuzi na biashara.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN pia amekutana Makamu wa Rais wa TIGO – Afrika RACHEL SAMREN ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo namna kampuni hiyo itakavyosadia katika kuwawezesha wanawake kuondokana na umaskini hapa nchini.

Katika kuhakikisha taifa linaongeza ukusanyaji wa mapato,
Makamu wa Rais ameuhimiza uongozi wa kampuni ya Simu ya Tigo hapa nchini kuhakikisha unalipa kodi kwa uwazi ili fedha hizo ziweze kusaidia serikali katika kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na  Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala ,Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren (Kushoto) wakati Bi. Rachel Samren alipomtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala (kushoto) mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri asiye na Wizara Maalum katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo kinachoshughulikia masuala ya utendaji Na utekelezaji wa miradi ya serikali Dk. Sri Idris Jala na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Tigo Afrika Bi. Rachel Samren  wengine pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kisheria Bi. Sylvia Balwire na Bi. Halima Okash Afisa Uhusiano (wa kwanza kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 24 Juni 2016. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...