Mkurugenzi wa kampuni ya Ovans Construction Company Limited, ambao ni wamiliki wa Kusile Restaurant and Lodge, Valence Urio upande wa kulia akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru mara baada ya Kiongozi wa mbio za Mwenge George Mbijima kufungua rasmi hoteli hiyo iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, George Mbijimi akiondoa kitambaa ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa hoteli ya kisasa ya Kusile Restaurant and Lodge iliyopo Mbinga mjini mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa halmashauri ya ya mji wa Mbinga Bw. Oscar Yapesa (kushoto) akikabidhi mwenge wa uhuru jana kwa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini Bw. Venance Mwamenge mara baada ya kumaliza mbio zake katika mji wa Mbinga,
Show original message
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Georg Mbijima akiangalia ubora wa meza na madawati jana katika kijiji cha Mbuji wilayani Mbinga kabla ya kusambazwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani humo.
Mratibu wa elimu kata katika kata ya Litura halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini mkoani Ruvuma Nicodem Hyera akijaribu kuwasha moja kati ya pikipii zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili ya kuwawezesha waratibu elimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ziweze kuwasaidia kufuatilia maendeleo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari wilayani Mbinga. Picha zote na Muhidin Amri, Mbinga







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...