Na Geofrey Chambua
1.Ni
mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu.
Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa
maji pekee.
2.Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya
kunywa maji.
3.Wakati moyo wa mwanadamu ni mmoja wenye
chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.
4.Baadhi ya mende wa kike hawaitaji wanaume
kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi
chote cha maisha yao.
5.Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika
40 bila ya kupumua.
6.Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki
mbili akiwa amekatwa kichwa.
7.Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa
kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai.
8.Mende ni mdudu asiye na mapafu.
9.Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa.
10. Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia
sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof
Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda
roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.
11. Mende wanatumiwa pia katika matibabu.
Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda
mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa
wanatoa kemikali za kupigana na sumu. Leo katika hospitali Uchina, krimu
inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kutibu
vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...