Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha akizungumza na waandishi wa habari LEO kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa (special diet) wanaolazwa MNH kuanzia Julai Mosi, mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akifafanua jambo LEO katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hospitali hiyo kuanza kuboresha huduma ya chakula kwa wagonjwa. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Aminiel Aligaesha akiwa kwenye mkutano huo. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aligaesha akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari LEO jijini Dar es Salaam.

·         Yawaondolea usumbufu ndugu wa wagonjwa kupeleka  chakula mara tatu kwa siku.
·         Ndugu watapata muda wa kuendelea na shughuli za uzalishaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeboresha huduma za chakula kwa wagonjwa wote watakaolazwa kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ili kuwaondolea ndugu wa wagonjwa usumbufu na gharama za usafiri wakati wa wanapokwenda kuwaona ndugu zao waliolazwa mara tatu kwa siku katika hospitali hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma hiyo kwa wagonjwa wote wanaolazwa.
Kwanini Hospitali imechukua hatua hii
Bw. Aligaesha amesema Hospitali inataka kujikita katika majukumu yake ya msingi ambayo ni kushauri, kuchunguza na kutibu.

“Aidha Hospitali inataka kuwaondelea adha ndugu wa wagonjwa ambao wamekuwa wakiingia gharama kubwa hususani usafiri wa kuja Hospitalini mara tatu kwa siku, ambapo kwa kukadiria gharama ya usafiri wa ndugu mmoja wa mgonjwa ni kati ya shilingi 6,000/= na 10,000/= kwa siku, kulingana na mahali anapotokea bila kujumuisha gharama za kuandaa chakula cha mgonjwa ambacho mara nyingi ni chakula maalumu. Na kama mgonjwa akilazwa zaidi ya siku tano hadi 10 ndugu mmoja wa mgonjwa gharama atalipia fedha nyingi kwenye usafiri” amesema Bw. Aligaesha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2016

    hii sasa yanarudi yale yaleee...ya kupenyeza chakula kwa njia za kutoa rushwa....Mgonjwa hataki menu yao anataka chakula fulani ndicho anaagiza nyumbani. Au usiku wanamenu ya viazi mgonjwa huwa hapendi viazi ....Hii kazi sasa inaanza.

    Nahisi ni miradi ya watu hii..

    Kwanini wasifikirie kuboresha mazingira ya Kufanyia kazi madaktari, kuwaongezea mishahara wafanye kazi kwa furaha, Madawa yawe ya kutosha, n.k. wanakimbilia kufanya hili.

    Wakati walishalifanya tena miaka ya nyuma ikafeli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2016

    Asante sana, Mungu atawabariki...kuna watu hata mkiboresha vipi hawaoni.....wanaangalia mabaya tu. Keep up a good work

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...