Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase akitoa maelezo ya moja ya kifaa kinachotumika kwenye kivuko cha MV Magogoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulia Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua mradi huo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA) Eng. Le- Kujan Manase wakati alipokagua mradi wa ukarabati wa ujenzi wa vivuko vitatu jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Kivuko cha
MV. Magogoni kikiwa kwenye hatua za mwisho za matengezo yanayofanywa na kampuni
ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya Mwanza na TEMESA Jijini Dar es
salaam.
Picha
zote na Benjamin Sawe- Maelezo
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua ukarabati na Ujenzi wa
Vivuko vya MV. Magogoni na MV. Pangani na kuwataka wajenzi wa vivuko hivyo
kuhakikisha vinakamilika kwa wakati.
Akizungumza mara baada
ya kuvikagua Vivuko vya Old MV- Magogoni na Ujenzi wa vivuko vipya vya Pangani
na New Magogoni, Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na hatua za ujenzi
zilizofikiwa na kusisitiza kuwa upo umuhimu wa kazi hizo kufanywa hapa hapa
nchini badala ya kupelekwa nje ya nchi.
“Hakikisheni mnaongeza
nguvu na wataalam ili kazi zote za vivuko na ujenzi wa boti za kuongozea Meli
(Tag), zifanyike hapa hapa nchini na hivyo kuokoa fedha nyingi zinazotumika kila mwaka
kwa Tug zote saba kukarabatiwa nje ya nchi ”, Amesema Prof. Mbarawa.
Ameitaka Mamlaka ya
Bandari Tanzania (TPA) kutenga na kujenga eneo maalum litakalotumika kufanyia
ukarabati wa vivuko, matishali na boti za kuongozea Meli ili kuboresha huduma
ya ufundi katika vyombo vya majini.
“lazima kuwe na
mkakati wa kuokoa takribani dola Milioni mbili nukta tano zinazotumika kwaajili
ya ukarabati wa Tag zetu kila mwaka”, Amesisitiza Prof. Mbarawa.
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Eng. Le- Kujan
Manase amemweleza Prof. Mbarawa kuwa kazi zote za ukarabati wa vyuma na umeme
zinafanywa na Mkandarasi kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Courtyard ya
Mwanza na matengenezo ya Injini na mitambo ya kuendeshea Kivuko yanafanywa na
mafundi wa TEMESA na kazi zote zinatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwezi wa
nane.
Kukamilika kwa kivuko
cha Old Magogoni na Vivuko vipya viwili vya Pangani na New Magogoni
kutaiwezesha TEMESA kuwa na vivuko 30 vinavyotoa huduma hapa nchini na hivyo
kuboresha huduma hiyo katika maeneo mengi.
Katika hatua nyingine
Prof. Mbarawa amewataka wenye malori yanayoengeshwa pembeni ya barabara ya
kuiingilia Bandarini kutafuta mahali pengine pa kuegesha magari hayo ili
kuondoa usumbufu kwa wasafirishaji wanaoingia na kutoka bandarini.
Kivuko kipaya cha
Pangani kinatarajiwa kukamilika mwezi septemba na kile kipya cha Magogoni mwezi
Oktoba mwaka huu.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...