Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

UONGOZI wa klabu ya Azam umeweka wazi kuanzia Julai 01 watataja majina ya wachezaji watakaoachwa na timu hiyo pamoja na wanaotarajiwa kujiunga nao, hilo linakuja katika kuimarisha kikosi hicho chenye maskani yake Chamazi hasa baada ya kushindwa kufikia malengo waliyoyaweka ya kucheza klabi bingwa Afrika mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habaru, Afisa habari wa Azam, Jaffari Iddy Maganga amesema kuwa wanataka kutengeneza kikosi ambacho kitakuja kuwa na ushindani mkubwa na kufikia malengo waliyojiwekea hususani kucheza klabu bingwa na kufika mbali zaidi. "Azam tumetolewa mapema kwenye kombe la Shirikisho tuhakamishia nguvu zetu kwenye ligi lakini tukaishia kushika Nafasi ya pili".

Amesema Jaffari, Julai Mosi wataweka wazi wachezaji watakaowaacha kwenye timu ya wakubwa na ni wachezaji wangapi wataongezwa kutoka timu ndogo ikiwa pamoja kuwataja wachezaji watakaosajiliwa ili kuboresha kikosi chetu.

"Tutawatumia zaidi wachezaji wetu wa kikosi B kwani umefika muda wa kuwapa nafasi za kucheza timu kubwa kwani wameonesha uwezo wa hali ya juu sana katika michuano ya vijana na wana uwezo mkubwa,"amesema.

Ukiachilia hilo, amewataka mashabiki wa Azam kuwa na subira na kuacha kusikiliza maneno ya watu zaidi ni kuwa wachezaji kwa sasa wapo mapumziko ila watarejea hivi karibuni kwa ajili ya kujiunga na kuanza mazoezi ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...