Yanga yanasa mshambuliaji mwingine baada ya kupata saini yake kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili. Obrey Chirwa mwenye asili ya Zambia aliyekuwa anakipiga kwa wachimba madini FC Platinum ametua leo jioni na usiku huu kumalizana na Wanajangwani hao na anatarajiwa kuungana na wenzake siku ya Jumapili kwa ajili ya kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Mabingwa hao wa ligi kuu Vodacom, wamekuwa katika mikakati ya kuimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji watakaoweza kusaidia timu yao kwenye michuano iliyokuwa mbele yao pamoja na ligi kuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...