Jaji Francis  Mutungi  amekutana na watumishi kutoka ofisi yake na kupata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi ya kila siku ikiwa ni moja ya shughuli katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma. Pichani akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. 
Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano  wa watumishi.


Katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma yenye kauli mbiu“uongozi wa umma kwa ukuaji jumuishi: kuelekea katika afrika tunayoitaka” Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi jana amekutana na watumishi kutoka ofisi yake na kupata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi ya kila siku.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo uliopo kivukoni Ilala, Mtaa wa Shabani Robert jijini Dar es salaam.

Akitoa majibu ya baadhi ya changamoto hizo, Jaji Mutungi aliwashukuru watumishi wote  kwa kazi  nzuri ya kulijenga taifa  na amewataka  watumishi hao kufanya  kazi kwa uaminifu, ueledi  na kwa bidii zaidi ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

“Serikali ina dhamira nzuri katika kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo tunapaswa kuhakikisha kwamba dhamira ya Serikali inatekelezwa kwa vitendo” alisisitiza Jaji Mutungi

Kwa upande wao watumishi wameiomba Serikali kuona namna nzuri ya kushughulikia changamoto mbali mbali za watumishi .
Siku hiyo maalumu ya kusikiliza changamoto na maoni ya watumishi ni utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa agizo la Serikali katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23, 2016.

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pia imetenga siku ya kesho  Ijumaa ya tarehe 24  Juni, 2016 kwa ajili ya kukutana na wadau wake kwa lengo la kutoa elimu na kupokea changamoto wanazokumbana nazo wadau hususani katika  masuala yanayohusu Vyama vya Siasa na sheria zake .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...