Jeshi la Polisi limesema kuwa ongezeko la makosa ya watumiaji wa barabara limechangia jeshi hilo kuagiza askari wake kukamata watumiaji kumi kila siku wanaovunja sheria za barabarani.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Kikosi cha usalama barabarani Mohammed R. Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Mpinga amesema kuwa kumekuwa na ongezekezo kubwa la uvunjifu wa sheria za barabarani kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka huu ambapo katika kipindi hicho makosa 290,161 zaidi yaliyokamatwa tofauti na mwaka jana.

Alisema kwa kipindi cha Januari hadi Mei 2015 jumla ya makosa 484,034 yalikamatwa nchi nzima wakati kwa kipindi cha Januari mpaka Mei 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa Tanzania bara.

“Kwa mfano kwa kipindi cha Januari hadi Mei mwaka 2015 jumla ya makosa ya usalama barabarani 484,034 yalikamatwa katika mikoa yote Tanzania Bara na kwa kipindi kama hicho cha Januari hadi Mei mwaka 2016 jumla ya makosa 774,195 yalikamatwa pia katika mikoa yote Tanzania Bara” alisema Kamanda Mpinga.

Akizungumzai hoja ya kuweka kiwango cha ukamataji wa makosa kwa askari wa jeshi hilo, Kamanda Mpinga alisema kuwa Polisi haiwezi kuweka idadi ya makosa ya kukamata wakati madereva wanaendelea kufanya makosa barabarani na ajali zinaendelea kutokea.

“Askari wameelekezwa wakamate makosa mengi iwezekanavyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba madereva wengi Barabarani hawazingatii sheria za Usalama Barabarani hivyo kusababisha ajali,” alisema Kamanda Mpinga.Aidha Kamanda Mpinga amewatahadharisha madereva wote kuacha kufanya makosa Barabarani kwani Jeshi la Polisi halitawavumilia, litawakamata na kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Makosa yanayofanywa na madereva wengi ni pamoja na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari (Overtaking), kupita taa nyekundu, kuendesha kwa mwendo kasi, kuendesha wakiwa wamelewa, madereva bodaboda kutovaa kofia ngumu, kubeba mishikaki, kutokuwa na leseni na pikipiki kutokuwa na Bima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...