Na Jonas Kamaleki 

Serikali imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.

Hayo yamesemwa leo Bungeni  mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango wakati akitoa hotuba kuhusu taarifa ya hali ya uchumi nchini na mpango wa maendeleo wa taifa 2016/17.

Waziri Mpango amesema kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ya serikali na kuongeza kuwa fedha za ndani ni shilingi bilioni 8,702.697 ambazo ni sawa na asiliia 74 ya bajeti ya maendeleo na fedha za nje ni shilingi bilioni 3,117.805 sawa na aslimia 26 ya maendeleo.

Aidha, Mpango amesema kuwa sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuanzisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango huo.

“ Kwa ujumla fedha za maendeleo zimeelekezwa zaidi katika miradi inayolenga kuendeleza viwanda kama vile uchukuzi,ujenzi, nishati, kilimo, maji, elimu na afya,”amesema Waziri Mpango.
Ameongeza kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 umeainisha miradi mikubwa ya kielelezo ambayo itapewa msisitizo katika utekelezaji wake.

Waziri Mpango ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma, mradi wa chuma Liganga, ujenzi wa reli mpya kati ya Dar – Kigoma na Tabora- Mwanza na matawi yake Isaka- Kigali/Keza- Msongati na Kaliua- Mpanda kwa kiwango cha standard gauge.

Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 utategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Phillip Mpango akiwasilisha bungeni Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwelekeo wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Shally Raymound (kulia) na Mary Mwanjelwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kamishina Valentino Mlowola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2016.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akiteta na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Zamaradi Kawawa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 8, 2016.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Wabunge wa Viti Maalum (CCM) wakiongozwa na Mhe. Margaret Sitta wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi cha bunge hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...