Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa kusaini mkataba na wazabuni 10 wa kutengeneza mdawati 28000 leo jijini Dar es Salaam.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Jacob  Boniface akisaini mkataba  wa kutengeneza madawati na  Mkurugenzi wa Kampuni ya Edosama Hardware,  leo jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya watu waliokuwa wakishuhudia utiaji saini wa mkataba wa kutengeneza madawati wa shule za msingi na Sekondari katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar  es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imekata posho za watendaji wa idara zake kwa muda wa miezi miwili  na kuweza kupata sh.bilioni 1.8 ambazo zitamaliza tatizo la madawati 28000 kwa shule za msingi na sekondari kwa manispaa ya Kinondoni.

Kuondosha kwa posho hizo kulitokana na manispaa  kubaini kuwa hawana uwezo wa kununua madawati 28000  kwa kukosa bajeti hiyo katika mwaka fedha 2015/2016  na kuona posho za watumishi zitumike kununua madawati hayo.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, wakati wa kusaini mkataba  wa kampuni 10 za kutengeneza madawati  28000, Meya wa Manispaa Kinondoni, Jacob Boniface amesema kuwa kwa kuingia mkataba huo kinondoni inachana na tatizo la madawati.

Jacob amesema kuwa Kinondoni wanafunzi kukaa chini ni aibu kutokana na Halmashauri hiyo kuwa na vyanzo mapato vingi.
Amesema kuwa waliongia mikataba kuhakikisha kufikia juni 30 mwaka huu wazabuni wote kuwa wamekamilisha utengenezaji wa madawati.

Jacob amesema kuwa madawati yanayokusanywa na wadau mbalimbali wanayahitaji kwa ajili kuweka akiba ili yakiharibika kuweza kutumika pale penye upungufu.

Ameasema madawati hayo yanatengenezwa kwa bei ndogo kuliko na awamu zote kwani kwa sasa yanatengenezwa kwa sh.85000, wakati kwa manispaa hiyo ilishatengeneza dawati moja kwa sh.400,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2016

    Huyu diwani yuko makini. Nependekeza apewe nafasi zaidi. Lakini sasa shughulikia kituo cha mabasi cha ubungo. Tumechoka kulipa ushuru bila kuona mabadiliko. Mvua ikinyesha abaria wananyeshewa. Hii si haki hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2016

    Kama wenye posho walishirikishwa bila shuruti hakuna tatizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...