Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo la Riverside.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo ‘mzee wa upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuhudhuria  ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini (hawapo pichani ) wa kanisa hilo la Maombezi la Mzee wa Upako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...