Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefuta hati ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya 5,000 yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori ambayo hayaendelezwi kufuatia malalamiko ya wakazi wa zaidi ya 2,000 wa kijiji cha Kibaranga kuhangaikia maeneo ya kilimo na kusababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni shamba la sita kufutwa na kuwapa wananchi na Mheshimiwa Rais katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema Serikali ya mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo na watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu utakaowezesha kila mwananchi apate shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza wananchi.

Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama Mheshimiwa Adadi Rajab amesema watahakikisha wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akiwatangazia wanakijiji wa Kibaranga kuwaelezea uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli wa kufuta hati ya Shamba leyenye hekta zaidi ya 5,000 ambalo lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

Wakazi wa kijiji cha Kibaranga wakielezea furaha yao kwa Mhe. Lukuvi kwa uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji kwa muda mrefu.
Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga kilipo kijiji cha Kibaranga, Mhe. Adadi Rajabu akizungumza baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuwaelezea wanakijiji hao uamuzi wa Rais Dk John Pombe Magufuli kufuta hati ya Shamba lililokuwa limetelekezwa na mwekezaji, kwenye kijiji cha Kibaranga kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...