Na: Lilian Lundo,MAELEZO
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino
yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa
chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini (Tanzania Albinism Society)
Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata
fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana
potofu hususani ushirikina.
“Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016
yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo huduma za afya hususani
uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi
na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi
ya ulemavu,” alisema Temba.
Temba aliendelea kuainisha kwamba siku hiyo itawapa fursa watoto
wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa
Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la
UNICEF.
Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt.
Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera,
Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja
bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba
akizungumza na waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAS
Dar es Salaam, Gabriel Aluga, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba na Mratibu kutoka asasi ya
kiraia ya BADEF.
Mwenyekiti wa Mfuko wa Good Hope Star na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya
maadhimisho ya siku ya Albino duniani Al Shamaymaa Kwegyir akifafanua jambo wakati wa
mkutano wa waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kuliani Mwenyektiwa TAS Dar
es Salaam, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba (kushoto) na Mwenyekiti wa TAS Taifa
Nemes Temba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...