Jamaica ni timu ambayo haijafunga bao hata moja katika michuano hii ya Copa Amerika mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka jana, baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uruguay kwenye mchezo wa mwisho wa kundi C uliopigwa ndani ya dimba la Levis Stadium,Santa Clara, Califonia.

Mabao ya Uruguay yalifungwa na Abel Hernandez kunako dakika ya 21,baadaye Jeh Vaughn Watson wa Jamaica akajifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa.Wakati mpira ukielekea kumalizika yaani dakika 2 kabla ya kipyenga cha mwisho kupulizwa Mathias Corujo akaipatia Uruguay goli la 3. Pamoja na ushindi huo Uruguay nayo imeaga mashindano.
Lakini katika mchezo uliotangulia kwenye dimba la NRG Stadium,Houston,Texas, watazamaji wapatao 67,319 walishuhudia timu za Mexico na Venezuela zikienda sare ya kufungana bao 1-1. Timu zote hizi mbili zimetinga hatua ya robo fainali.

Walikuwa ni venezuela walitangilia kujipatia bao kunako dakika ya 10 ya mchezo kwa goli zuri la mpira wa 'VOLLEY' na kiungo mshambulizi Jose Velazquez. Kipindi cha pili kunako dakika ya 79 Jesus Corona wa Uruguay aliwachambua chambua wachezaji wapatao saba wa Venezuela akawafungasha tela kisha kuachia mkwaju mkali uliokwenda kimiani na kuisawazishia Mexico bao.

Leo itahitimishwa michezo ya kundi D

PANAMA vs CHILE
ARGENTINA vs BOLIVIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...