
Wafanya kazi wa Jumuia ya Muzdalifat wakitayarisha malipo ya Msaada kwa ajili ya Watoto Mayatima wanaosaidiwa na Shirika la Misaada la I,H,H,INSANI YARDIM VAFKI kutoka Uturuki, hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile selasi mjini Unguja.

Baadhi ya Watoto mayatima wanaopatiwa Fedha za Msaada na I,H,H,INSANI YARDIM VAFKI kutoka Uturuki,wakishirikiana na Jumuiya ya Muzdalifat wakiongozana na walezi wao kuchukua fedha zao.Zaidi ya watoto 800,wamepatiwa fedha hizo katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi mjini Unguja.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifat Farouk akizungumza machache katika hafla ya kuwa kabidhi Fedha Watoto Mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja.

Mfanyakazi wa Jumuiya ya Muzdalifat akiwakabidhi Watoto mayatima Wanao fadhiliwa na Shirika la I,H,H INSANI YARDIM VAKFI la uturuki,Fedha taslim za msaada katika ukumbi wa Skuli ya Haile Selasi Mjini Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...