TAASISI ya Benjamin W. Mkapa (BMF) leo imesaini mkataba wa miaka mitatu na shirika lijulikanalo kama Tropical Health Education Trust (THET) wa kusimamia mradi uliolenga kuisaidia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuweza kuzalisha kada mbalimbali za wahudumu wa Afya katika Jamii.
Mradi huu ambao unagharimu Tsh. 3.3 bilion, umefadhiliwa na shirika la kutoa misada la Uingereza lijulikanalo kama Comic Relief, unalenga kutekeleza sera za mbalimbali ya afya nchini, kujengea uwezo wahudumu wa afya katika jamiii kupitia mafunzo stahiki kuanzia ngazi ya mkoa, wilaya mpaka kanda. Vilevile kuajiri na kuwabakiza wahudumu hao wa afya katika ngazi ya jamii.
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa (BMF) yasaini mkataba na shirika la Tropical Health Education Trust (THET) kutekeleza mradi wa Huduma za Afya za kijamii.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Maendeleo ya Mradi wa miaka mitatu ambao utashirikisha vyou vya afya ya jamii pamoja na hospitali za rufaa za kanda ya ziwa pamoja na kusaini mkataba ya makubaliano ya kuendesha mradi wa wataalamu wa afya ya jamii pamoja na watu wa kada ya afya wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro amesema, “Mradi huu utasaidia Serikali kupunguza tatizo la uhaba wa watumishi wa afya ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji tunategea kuzalisha wahudumu wa afya katika ngazi ya jamii ambao watakuwa na ujuzi stahiki utaowawezesha kutoa huduma bora kwenye jamii husika. Na kwa ushirikiano na Wizara ya Afya pamoja na uongozi wa makoa na halmashuri za Kanda ya Ziwa, tunategemea ongezeko la utumiaji wa huduma za afya kwenye jamii.
Dkt. Ellen amesema kuwa mradi utatekelezwa katika vyuo vya afya 10, hospitali 4 za rufaa na kituo cha rasilimali 1, vyote hivyo viko katika mikoa 5 ya Kanda ya Ziwa nayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Kagera na Shinyanga.
Vyuo hivyo vilivyopo mikoa ya kanda ya ziwa vya kada ya afya ni Bukumbi school of Nursing, Ngudu School of Invironmental Health, Tandabui Institute of HST, Geita Nursing & Midwifery School, Bishop Kisula College of HS, Rubya Health Training Institute, Karagwe Institute of Allied Health Sciencies, Murugwanza School of Nursing, Kahama SON, Kolandoto of Nursing na Hospitali za Rufaa za kanda ya ziwa zitakazo fikiwa na mradi huoni Sekou Toure Geita Regional Referral Hospital, Kagera na Shinyanga.
Kuanalia uhaba wa watumishi wa afya.
Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika akizungumza jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusaini Mkataba wa kushirikiana katika kutoa mafunzo ya afya ya jamii ili kupunguza uhaba wa wafanyakazi wa kada ya afya hapa nchini.
amesema kuwa kupitia mradi huo wataalam wa afya ya jamii wataongezewa ujuzi pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kanda ya ziwa watapata ujuzi ambao utakua unastahili. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakisaini mkataba kati Taasisi ya Mkapa na Tropical Health Education Trust(THET) kwaajili ya kutoa mafunzo kwa wananchi wa kada ya Afya ya Jamii pamoja na wafanyakazi wa kada ya afya waliopo katika huspitali zilizopo hospitali za rufaa za kanda ya ziwa.
amesema “Tanzania inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya mojawapo ikiwemo upungufu wa rasilimali watu katika sekta ya Afya, ambapo upungufu uko kwa 52%. Tuna imani kwa kuongeza watumishi wa Afya kwenye ile mikoa yenye uhitaji Zaidi kutasaidia kupunguza changamoto mbalimbali za kiafya zinazoyakabili maeneo haya ikiwemo maambukizi ya VVU pamoja na vifo vya wamama na watoto.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Ellen Mkondya-Senkoro (Kushoto) na Meneja Mwakilishi Mkazi wa Tropical Health Education Trust(THET) Tanzania, Godwin Kabalika (Kulia) wakibadilishana mikataba jijini Dar es Salaam leo, Kwaajili ya mradi ambao umaeshirikisha Taasisi pamoja na serikali kwaajili ya kusaidi wataalam pamoja na wanafunzi wa kada ya afya hapa nchini.
Taasisi ya Mkapa na THET wametoa rai kwa wadau wote ambao wako katika sekta ya afya hususani wale wanaosaidia kuboresha rasilimali watu Afya kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kutekeleza mipango madhubuti ya afya ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali. Vilevile kwa halmashauri husika kutenga bajeti kwaajili ya huduma za kijamii ikiwemo mishahara ya watumishi wanaotoa na wanaotegemewa kuja kutoa huduma kwa jamii kuweza kufanya program kuwa endelevu.
Taasisi ya Mkapa na THET wametoa rai kwa wadau wote ambao wako katika sekta ya afya hususani wale wanaosaidia kuboresha rasilimali watu Afya kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kutekeleza mipango madhubuti ya afya ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali. Vilevile kwa halmashauri husika kutenga bajeti kwaajili ya huduma za kijamii ikiwemo mishahara ya watumishi wanaotoa na wanaotegemewa kuja kutoa huduma kwa jamii kuweza kufanya program kuwa endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...