Taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa mara nyingine tena, wamefika mkoa wa Mtwara, kukabidhi kona za kusomea (Reading Corners) katika shule mbili, Lilungu na Nanguruwe. Jumla ya vitu walivyokabidhi ni madawati 60, makabati ya vitabu 4, vitabu 181, chati za mfano, herufi, hisabati pamoja na vifaa vya sanaa kama rangi za kuchorea, na kadhalika. 

Mchango huu ni sehemu ya mradi wa DAWATI KWA KILA MTOTO (A Desk For Every Child) ambao umedhaminiwa na Shirika la marekani 'We are the world kids kama sehemu ya mpango wao wa kimataifa kujenga na kuanzisha maktaba na kona za kusomea kwa ajili ya shule za msingi na sekondari katika afrika na mashariki mwa Asia.'
Mgeni wa heshima katika sherehe hii ni Mh. Halima Dendego -Mkuu wa Mkoa Mtwara, akiongozana na Mh.Fatuma Ally - Mkuu wa Wilaya Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...