Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu ni chimbuko la  dojo iliyo jengwa na Master Eiichi Miyazato miaka 63 iliyo pita huko mjini Naha, Okinawa baada ya  kifo cha mwanzilishi wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu , Master Chijun  Miyagi , ambayo hivi sasa  inaendeshwa na mtoto wake Yoshihiro Kancho Miyazato.
Sensei Rumadha Fundi, alipokea na kukubali mwaliko kama mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Tanzania akiwa natumaini la usajili wa chama hicho hapa Tanzania.
Hivi karibuni Sensei Rumadha alikuwa  nchini Ureno hivi sasa kuishiriki katika kongamano la Karate " European Jundokan  Gasshuku 2016". 
Na wakati huohuo, kitengo kinachisimamia ubora na uthabiti wa  sanaa asili ya mitindo ya  karate toka Okinawa kiitwacho " OKINAWA BODOKAN & KARATE FEDERATION" kimefanya mabadiliko hivi karibuni yatakayo tofautisha  karate asilia na ile ya  kimichezo itayo kuwa katika michezo ya  Olympics.
Kutokana na mabadiliko ya  kimbinu na ufasaha yanayoonekana katika michezo, shirikisho hilo limeamua kutofautisha kabisa jinsi karate asilia izidi kuimarika na kutochujwa na kuwa sanaa nyepesi.

Pia, kuhakikisha  kiundani zaidi kwamba  mbinu halisi zinazingatiwa na ma- Sensei wote wa mitindo ya  karate toka visiwani Okinawa duniania kote. 
Hivyo imeteuliwa timu ya Karate ya Okinawa ( Masters) toka mitindo mbalimbali inayotambulika na " BUDOKAN" kusambaza uadilifu wa mitindo hiyo kama jinsi ilivyokuwa  inafundisha na waasisi wake asilia.

Semina hii inayoendelea nchini Ureno inawawezesha walimu ( Sensei) kuwa na mabadiliko au kuendana sambamba na jinsi sanaa inavyo jadiliwa katika chimbuko lake chini ya shirikisho hilo huko Okinawa,Japan.
Inatumainiwa  kwamba chama cha "JUNDOKAN SO HONBU" kitapata usajili wake nchini Tanzania pasipo fika mwaka 2018, chini ya Sensei Rumadha Fundi mwakilishi wa "JUNDOKAN SO HONBU" Afrika mashariki na Kati. "Endapo usajili utalegalega na kuvuta muda zaidi, basi chama hicho hakitakuwa na budi, bali kitajisajili visiwa vya Zanzibar kwanza" amesema sensei Rumadha.
 Yoshihiro Miyazato, mkuu WA Jundokan duniani, na Sensei Rumadha
 Tuka shoto ni  Tsuneo Kinjo sensei 9 Dan , OKINAWA  BUDOKAN " Certified overseas trainer", Gima Sensei 9 Dan , OKINAWA BODOKAN "Overseas trainer, Yoshihiro Miyazato, mkuu wa Jundokan duniani, na Sensei Rumadha.
 Sensei Rene , miaka 78 anaishi Paris kwa zaidi ya miaka 45 sasa ni mzaliwa wa Madagascar,  anashikilia Dan 8 toka Jundokan Karate. Pia ana dojo na wanafunzi wenye  ngazi za juu za  Karate huko Madagascar.

Miyazaki Sensei 5 Dan, aliyekulia katika Jundokan dojo tokea yupo shule us vududu " Kindergarten" huko Okinawa, Sensei Rumadha kati na Sensei Kinjo kulia.

Picha ifuatayo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...