Hivi ndivyo lionekanavyo Daraja la Mungu lililopo nje kidogo ya Mji wa Kiwira, Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, ni Daraja ambalo lilijitengeneza lenyewe kwa maajabu ya Mungu na hakuna mtu au mafundi walio husika katika ujenzi wa daraja hilo.
Baadhi ya wenyeji wa eneo lililopo Daraja hilo, wanasema kwamba kipindi cha nyuma (yaani enzi za mababu zetu) walikuwa wakihangaika sana kujenga daraja katika eneo hilo na jitihada za ujenzi wa daraja katika eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kutokana na kila walipokuwa wakijenga wanakuta pana bomoka bila ndoto yao hiyo kutimia.
Ila siku moja wa walipo rudi tena kuendelea na ujenzi wa daraja lao, ndipo walipolikuta daraja hilo lililo jitengeneza kwa miujiza ya Mungu, ndipo hapo lilipopewa jina la Daraja la Mungu.
Daraja hilo lenye ukubwa wa aina yake lililo katiza juu ya maji katika mto wa Rungwe linapitisha watu kwa kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Pichani ni sehemu ya pili kutoka juu ya Daraja hilo la Mungu ambapo maji yake huwa yanatowa mvuke muda wote.
Sehemu ya upande mwingine wa daraja hilo la Mungu kukiwa na daraja lingine lililojengwa baadae.
Upande wa chini wa daraja lingine lililo jengwa na binadamu lipo Sanjari na Daraja la mungu.
Hii ni moja ya alama yenye kuonyesha tarehe ya mtu mmoja mwenye asili ya India anae sadikiwa kupoteza maisha juu ya daraja hilo kwa kukosea masharti ya daraja hilo miaka ya nyuma, hivyo baadhi ya wahindi huja katika eneo lilipo jiwe hili na kufanya ibada zao. jiwe hili lipo juu ya daraja la mungu.
Muonekano wa daraja lilojengwa na watu lililopo mkabala na daraja hilo la mungu.PICHA ZOTE NA MR. PENGO WA MMG, Nyanda za Juu Kusini.
Basi liwekewe kinga ili watu wengine waianguke na kupoteza maisha
ReplyDelete