Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
KOCHA mkuu wa timu ya walemavu ya Tenisi, Riziki Salum amesema kuwa timu yake ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya kuelekea michuano ya wazi nchini Kenya na kujihakikishia kuwa watarejea na ubingwa huo kwa mara nyingine tena kwani watahakikisha wanatetea taji hilo.
Tunachokiamini kuwa wachezaji saba wachanga tuliokuwa nao tukijumuisha na wakongwe kama Novatus Temba tunaahidi kurudi kifua mbele.
Amesema, kwa rekodi waliyoiweka toka 2013, walipochukua timu bora ya mwaka kwenye kombe la Dunia nchini Uturuki na waliposhiriki kwenye michuano ya mataifa nane Afrika Kusini 2014 na kuchukua nafasi ya pili yanawapa nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya vizuri zaidi wao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya wazi ya Kenya.
"Tuna wachezaji wazuri ukichukua chipukizi na mkongwe Novatus Temba na wamenihakikishia kufanya vizuri zaidi ukiangalia rekodi yetu ni nzuri, 2013 tumekuwa timu bora Duniani katika kombe la Dunia, 2014 tumeshiriki mashindano yaliyohusisha mataifa nane nchini Afrika ya Kusini na tukashika nafasi ya pili na ukizingatia tunaenda tukiwa mabingwa watetezi ,"amesema Salum.
Ametoa wito kwa wazazi kuwapa fursa watoto wao zaidi kwani kuwa mlemavu sio chanzo cha kushindwa kujumuika na wenzake kwenye michezo mingine na hata hivyo amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuja kusaidia mchezo huo hususani kwa walemavu kwani timu hiyo imeweza kufanya vizuri lakini hakuna wanaoangalia zaidi ya Mpira wa miguu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...