Wananchi wameipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa ufanisi wake katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kwa manufaa ya Taifa.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi mbalimbali kwa nyakati tofauti waliofika katika Uwanja wa Makao Makuu ya Ofisi za Wizara ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

Mmoja wa wananchi waliotoa pongezi hizo, Abdulhamid Jumaa alisema wizara imejitahidi kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika.

“Kwakweli mnajitahidi sana, sasa hivi tatizo la kukatika katika kwa umeme limemalizika, nawapongeza ila msibweteke tukajikuta tumerudi nyuma.”

Mwaka huu Wiki ya utumishi wa Umma imeadhimishwa kwa viongozi wa Wizara kusikiliza kero na maoni ya wananchi ambapo wananchi mbalimbali walipata fursa ya kueleza kero zinazowakabili na kuzungumza na Wataalamu mbalimbali.
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini - Idara ya Madini, Mhandisi Chacha Marwa (kushoto) na Mhandisi Chiku Juma wakimsikiliza Hussein Jafari (kulia) akitoa maoni yake kuhusu uboreshwaji wa uchimbaji mdogo wa madini nchini.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati sehemu ya Gesi Asilia, Ebahart Diliwa akinakili hoja na ushauri uliokuwa ukitolewa na mwananchi George Mgaya (kulia) ambaye alifika wizarani hapo ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
Mtaalamu kutoka Idara ya Sheria Wizara ya Nishati na Madini, Phines Sijaona (kushoto) akimfafanulia jambo Alli Hamisi ambaye alifika wizarani hapo kwa lengo la kuwasilisha hoja na ushauri kuhusu masuala mbalimbali ya nishati na madini.
Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Leseni, Mhandisi John Nayopa (kulia) akizungumza na Mwandishi wa Habari wa Azam Tv, Estabella Malisa (kushoto) kuhusu muitikio wa wananchi wa kutoa hoja na ushauri kuhusu shughuli za wizara katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Ofisi ya Wizara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...