WAZIRI wa Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana kuwachukulia hatua watendaji wote waliosimamishwa kati katika wizara ya elimu pamoja na kuwafikisha vyombo vya dola. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu- Elimu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leunard Akwilapo.
Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Tarish Kibenga Katikati Naibu Katibu Mkuu- Sayansi na Ubunifu, Simon Masanjila na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Wizara Elimu, Sayansi na Teknolojia, Anna Mhere.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ametangaza kiama kwa
watendaji wote wa Bodi ya Mikopo
waliofanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu
wasiohusika.
Joyce ameyasema leo wakati
akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo. amesema kuwa bodi ya
mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni hoja moja imepata
majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi
kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.
Amesema kuwa kutokana na matatizo ya
bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha wanachukua hatua kwa watendaji wote
waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha vyombo vya dola.
Joyce amesema kuwa katika dosari
nyingine wanafunzi zaidi 2,000 wamepewa mikopo katika vyuo viwili lakini
wanafunzi hao hawapo katika vyuo vilivyotajwa.
Amesema kuwa kuna wanafunzi wanalipwa
sehemu mbili ya mikopo ya bodi kwa
Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati mikopo kabisa na watoto wa masikini.
Aidha amesema bodi hiyo inatakiwa
kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua ambazo wamezichukua kwa baadhi ya
watendaji ambao wamefuja fedha za walipa kodi.
Joyce amesema kuwa matatizo mengine
ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Elimu
na ufundi (NACTE) kufanya kazi kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo
ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.
Amesema yote wanaangalia kwa kupitia
sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE kufanya kazi kwa
uwezo unaostahili.




Endelea kusafisha huu ubadhilifu siyo endelevu usingetufikisha popote ila kutufunga na madeni zaidi na kuwanyima huduma wale wanaostahili.
ReplyDelete