KATIKA kusherekea siku ya mtoto wa Africa, Bank ya CRDB Tawi la Water Front limetoa zawadi mbali mbali kwa watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo pamoja na kula keki pamoja na kunywa vinywaji nao, Katika kusherekea siku hii adhimu na muhimu.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wengine waliowafungulia akaunti katika benki hiyo amewanashkuru sana kwa kuwapa zawadi watoto wao na iwe chachu kwa wazazi wengine kuafungulia akaunti watoto wao.
Keki na zawadi kwaajili ya watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo katika Benki ya CRDB tawi la Water Front.
Watoto wakinyoosha mkono kujibu maswali ya Meneja wa Tawi la Water Front, Donath Sheirima jijini Dar es Salaam leo. Pia waliojibu maswali vizuri wamepewa zawadi mbalimbali ambazo zilikuwa zimeandaliwa kwaajili ya watoto hao katika tawi hilo.
Meneja Rasilimali watu wa Benki ya CRDB makao makuu, Timoth Fasha akikata keki kwaajili ya watoto wenye akaunti ya Junior Jumbo katika Tawi la Water Front jijini Dar es Salaam leo.
Watoto na wazazi wakifurahia Shampein ilivyofunguliwa jijini Dar es Salaam leo.
Watoto wakilishwa keki.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Water front akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi, wazazi na watoto wenye akaunti za Junior Jumbo katika tawi hilo jijini Dar es Salaam leo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.









Kama ni kupromote akaunti za watoto katika platform hii naona mmeshinda CRDB. Ni vizuri kuwawekea watoto akiba.
ReplyDelete