Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.
WATU wasiofahamika wanatuhumiwa kuchoma nyumba moja moto kwa kutumia petroli wilayani nyamagana.
KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio la kuchoma nyuma lilitokea Juni 13 mwaka huu majira ya saa 2 katika shamaliwa ,wilaya ya nyamagana katika makazi ya samson kaijunga (60).
Msangi amesema wakati Samson akiwa amelala usiku na familia yake alistuka na kugundua nyumba yake ikiwa inawaka moto ulioanzia sebuleni na kuteketeza baadhi ya mali ambazo ni seti moja ya sofa, kabati, na mbao zilizoezekea paa la juu ya nyumba pamoja na jipsamu na vitu vingine vidogovidogo lakini moto huo haukuleta madhara kwa binadamu.
Kamanda Msangi amesema wakati familia hiyo ikiwa imelala watu wasiofahamika walimwaga petroli ndani ya nyumba sebuleni kupitia dirishani kisha wakawasha moto ulioanzia kuwaka sebuleni na kuanza kusambaa kwenye vyumba, ndipo wenyenyumba walipogundua na kupiga yowe za kutaka msaada ambapo watu walifika na kusaidia kuuzima moto huo.
Amesema chanzo cha tukio hilo bado halijajulikana, lakini linahusishwa na wivu wa kimapenzi kati ya mke mdogo anayeishi kwenye nyumba ambapo tukio hilo la moto limetokea na wake wenzake wawili ambao hawana maelewano mazuri, mpaka hivi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Moto huo bado hazijafahamika , jeshi la polisi bado linanendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana natukio hilo. juhudi za kuwasaka na kuwatia nguvuni wahalifu wa tukio hilo bado zinaendelea.
Msangi amewataka wito kwa wananchi wa jiji na mkoa wa mwanza wote kwa pamoja kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kuwatia nguvuni wahalifu hao ambao ni hatari na wanania ovu dhidi ya binadamu wenzao.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...