Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia waumini wa Kanisa katoliki  jimbo la Geita baada ya kuhudhuria sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo hilo, Flavian Kassala  zilizofanyika mjini Geita Juni 12, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Askofu wa Jimbo la Geita , Mhashamu Flavian Kassala  katika Ibada ya kusimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki la Geita Juni 12, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa katoliki katika sherehe za kumsimika Askofu wa jimbo la Geita, Flavian Kassala  (kushoto kwake) zilizofanyika kwenye kanisa kuu katoliki mjini Geita Juni 12, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


            WATANZANIA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUPIGA VITA   MATUKIO YA MAUAJI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania, viongozi wa dini zote kushirikiana kwa pamoja kupiga vita matukio maovu ya mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema anatarajia hali ya amani, usalama na utulivu inaendelea kuwepo nchini, hivyo wananchi hawana budi kushirikiana na kushikamana na Serikali katika kuhakikisha matendo maovu hayatokei katika maeneo yao.
Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumamosi, Juni 11, 2016) wakati  alipowasili mkoani Geita kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya kuwekwa wakfu Padre Flavian Kassala kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Geita.
“Mfano tukio la Mwanza watu wanavaa kanzu na wanaingia msikitini na kukuta wenzao wanafanya ibada kisha wakawachinja, hii haiwezekani kwa binadamu wa kawaida hivyo tushirikiane katika kupiga vita matendo haya,” alisisitiza.
Hivi karibuni jumla ya watu 15 waliuawa kwa kukatwakatwa na mapanga katika mikoa ya Mwanza,Tanga, Dar es Salaam  na Mara.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga amesema vitendo vya watu kuuawa kwa kukatwa mapanga vimepungua baada ya kuanzisha kampeni maalumu ya kukemea mauaji hayo.
Alisema katika kampeni hiyo wameamua kuwatumia walimu, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wauguzi ambao wamekuwa wakiwaelimisha wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina na badala yake wajikite katika masuala ya maendeleo.
                       
IMETOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

JUMAPILI, JUNI 12, 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...