Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene (Mb), Katikati akizungumza wakati  wa ziara  ya kukagua mradi wa mabasi yaendayo haraka  leo  jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kushirikiana na viongozi wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia leo  hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara katika maeneo ya makutano ya barabara na katikati ya jiji.

Pia amemtaka Makonda kuhakikisha anawaondoa ombaomba wote  walipo katika makutano hayo pamoja katikati ya jiji kuweza kusaidiwa na sio kuomba hawawezi kujikwamua na umasikini.

Simbachawene alitoa agizo hilo  leo  alipofanya ziara katika mradi wa Mabasi yaendayo haraka UDART na kudai kwamba bado kuna changamoto kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kutokana na watu  kushindwa kufuata sheria ambazo zimewekwa.

Amesema  lengo la kuwaondoa wafanyabiashara na ombaomba hao ni kutaka kuhakikisha kwamba jiji la Dar es Salaam linakuwa katika muonekano mzuri na usafi  na kuweza kufuta mbinu nyingine ya kuwasaidia kupitia mfuko wa TASAF.

"Kuanzia  leo  sitaki kumuona mfanyabiashara katika maeneo hayo ya makutano na pembezoni mwa barabara watafutieni utaratibu ambao utawafanya wakae maeneo  salama  kutokana kila manispaa ilivyoanisha "amesema Simbachawene.

Aliongeza kuwa anataka katika maeneo hayo kuwepo na askari saa  24 ambao watahakikisha hakuna mfanyabiashara atakayefanya biashara baada ya kuondolewa.
"Acheni kukamata mama ntilie nataka askari hao watumike kuwakamata wafanyabiashara hao wakae hapo saa  24" amesema Simbachawene.

Amesema kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya jiji  kunachangiwa na uwepo wa biashara zinazofanywa katika mazingira ambayo sio rasmi na ndia chazo cha uchafu.

Kwa upande wa usafiri wa Mabasi yaendayo haraka UDART,Simbachawene pia amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kufuata sheria na kuacha kutumia Barabara za mwendo haraka hususani pikipiki na maguta.

Amesema serikali imejipanga  kukabiliana na changamoto  foleni kusimamia utekelezaji wa barabara  za mabasi ya  mwendo wa haraka awamu ya pili unatarajia kuanza  mwakani.

Simbachawene amesema tayari wameshafanya tathimini na utatumia miaka miwili hadi kukamilika kwake pia wapo  katika mchakato wa kumtafuta mkandarasi kwaajili ya ujenzi.

Amesema awamu ya pili itaanzia katika Barabara ya sokoine kuelekea barabara  ya Kilwa hadi  Mbagala na kutakuwa na barabara  za juu katika makutano ya barabara  ya Kawawa na Nyerere,
Nae  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amemuahidi Waziri huyo kuwa watatekeleza maagizo yote na kuahidi kuanzia oparesheni hiyo  leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2016

    Usafi wa majiji yetu uwe pia katika kuongeza njia za kisasa za miguu (promenade)zenye green spaces na mikahawa (cafe) fu kwa ajili ya mapumziko na kuongeza muonekano mzuri wa mji narsa za biashara(open markets) na ajira. Kuwa na taa za barabarani za solar ili kuwe na uchumi wa masaa 24 katika halmashauri zote. Kuangalia uwezekano wa kuwa na waterfronts kama recreation na business area kwenye miji yote yenye ufukwe ili kuongeza fursa za uchumi na ajira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...