Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka akizungumza wakati wa uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao inayolenga kuboresha ufanisi utakaowawezesha kumudu nafasi za uongozi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kulia), akishikana mikono Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kulia), katika hafla ya uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi za Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa program ya Mwanamke wa Wakati Ujao jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka pamoja na baadhi ya wawakilishi wa makapuni yanayosapoti program ya Mwanamke wa Wakati Ujao (walioketi), wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya washiriki wa program hiyo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...