Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amewataka wananchi wa Jimbo lake kuwa na Imani naye kwani yeye ni miongoni mwa “Majembe” ya Rais wa awamu ya tano, Mh. Dk. John Pombe Magufuli hivyo kwa Wananchi wa jimbo hilo kuchagua mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani wameramba dume na watapata fursa mbalimbali kama walivyoahidiwa kipindi cha kampeni.
Dk. Kigwangalla amebainisha hayo katika ziara yake ya kushukuru wananchi wa Jimbo hilo la Nzega Vijijini kwa kumuwezesha kumchagua kurudi Bungeni kwa kura nyingi na pia kumpigia Rais Magufuli kwa kula za kutosha kuingia madarakani
“Ndugu zangu wananchi wa Kata ya Milambo Itobo na wale wa Kata ya Magengati ...Leo narejea hapa kuwashukuru kwa kunichagua kwenu. Nashukuru sana kwani kula zenu zimeweza kuniwezesha mimi kwa mara nyingine tena kurejea Bungeni na kuweza kuwawakilisha nyie katika vikao vya maamuzi hasa vile vya kimaendeleo. Na kutokana na uchapaji wangu wa kazi hata Rais ameniona mimi ni jemba na amenipatia moja ya nafasi za Uwaziri.
ameniteua kwenye Baraza lake la Mawaziri. Napenda kuwapongeza sana na pia naomba niwafikishie salama za Rais kwa kuweza kumpatia kura nyingi sana za NDIO…” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo wa wazi ambao watu mbalimbali walipata wasaha wa kushuhudia mkutano huo wa kutoa shukrani ambapo pia alitoa misaada mbalimbali ambayo aliahidi yeye mwenyewe kwa moyo wake hasa kwa vijana.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...