NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemain Jaffo amesema kuwa fursa za elimu ni nyingi katika
vyuo vya nje ya nchi na gharama zake ni nafuu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Jaffo
ameyasema hayo wakati wa maonesho ya biashara ya Kimataifa katika
Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere (Sabasaba) katika banda la Global
Education Link (GEL), amewataka Watanzania kutumia maonyesho ya Sabasaba
kuwa ni kipindi muafaka kupata mambo mengi kwa wakati mmoja likiwamo
suala la elimu katika vyuo vya nje.
Jaffo amesema kuwa, maonesho ya sabasaba ni kipindi pekee kwa taasisi mbalimbali na huduma zake zinatolewa bure.Aidha
amesema kuwa wazazi wanaotaka kuwasomesha watoto wao katika vyuo vya
nje ya nchi kwa gharama nafuu watumie fursa hiyo kupita katika banda la
Global Education Link (GEL) watapata taarifa mbalimbali.
‘’Serikali
ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imejipanga hivyo kama
wasaidizi wake lazima tujipange kuhakikisha kwamba tuangalie jinsi ya
kubadilika kwa kasi na kubadilika huko kwa kwa kasi lazima tuhakikishe
tuna teknolojia yakutosha kabisa kwanza kiushindani, tuanzishe vitu
ambavyo vitakuwa na soko kubwa”amesema .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik S.Mollel amesema kuwa vijana wanaopitia kampuni
yao hata baada ya kupata udahili na kwenda masomoni nje ya nchi, wana
utaratibu wa kufuatiliwa maendeleo yao ili mzazi aweze kuona thamani ya
fedha anayetoa kwa kusomesha mtoto nje ya nchi.
Mollel
amesema kuwa vyuo vya nje wanavyokwenda wanafunzi kuna wawakilishi
wanaofanya kazi moja kwa moja na GEL ya kufatilia mienendo ya wanafunzi
wao kwa kipindi chote wanachosoma na taarifa zao zinatumwa na kisha
mzazi kupewa taarifa za maendeleo ya mtoto.
Amesema
kuwa watoto wanaokwenda kusoma vyuo vya nje vinatambuliwa na TCU na
vinatambuliwa na bodi za nchi husika ili kuweza kumsaidia mtoto kuwa na
uhakika wa elimu na utaalam aliyopata katika vyuo hivyo.
Global
Education Link (GEL) inaangalia hali ya uchumi wa ndani kuwa mzazi
anaweza kumudu gharama hizo na hakuna tofauti na vyuo vya ndani.Anasema mtoto anayesoma nje wanaangaliwa kwa kila namna kuanzia ili kumuondolea mzazi usumbufu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Education
link (GEL), Abdulmalik S.Mollel akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemain Jaffo alipokuwa akiagana nae mara baada ya kulitembelea banda hilo.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...