Jeshi nchini Uturuki usiku huu limetangaza kwamba limechukua nchi, na kusababisha sintofahamu katika nchi hiyo. Waziri Mkuu wake Binali Yildirim ametngaza kuwa jaribio la uasi wa wanajeshi linaendelea katika taarifa yake kwenye TV ya Taifa. "Uturuki haitoruhusu aina yoyote ya jaribio la kuvuruga demokrasia", ameapa.
“Kuna watu wamechukua hatua isivyo halali nje ya utaratibu wa mamlaka", amesema Yildirim na kuongezea. "Serikali iliyochaguliwa na wananchi bado iko madarakani. Serikali hii itaondoka pale tu wananchi wakisema hivyo".
Globu ya Jamii inafuatilia haya na itakupasha kinachoendelea...



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...