Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla ya kusherekea miaka kumi ya letshego Tanzania limited jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wadau wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini wakati wa kusherekea miaka 10 ya kampuni yao.

Kampuni ya letshego Tanzania limited ikijulikana kama Faidika imesheherekea miaka 10 ya utoaji wa huduma za kijamii hapa nchini na kuzindua upya safari ya mabadiliko na msukumo wa ujumuishaji kwenye sekta ya kifedha kwa lengo la kuboresha maisha ya wananchi wa tanzania 

Akizungumza kwenye hafla hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa faidika, Mbuso Dlamini amesema wataendelea kutoa ufumbuzi wa kifedha utakaoboresha maisha na kuhakikisha ufumbuzi huo unaleta maana kwa watanzania .

Aidha Dlamini amesema watashirikiana na Serikali kuwajengea ujuzi wananchi na kuhamasisha mahusiano ya kimkakati kwa lengo la kumwinua mtanzania mwenye kipato cha chini pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiria mali kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

‘Ili kufanikisha lengo la ujumuishaji wa kifedha faidika imeanzisha ufumbuzi wenye lengo la kuboresha maisha kupitia upatikanaji wa mikopo ya kilimo ,elimu, afya na nyumba kwa watu wenye kipato cha chini, cha kati na wajasiriamali wadogo’, alisema Dlamini.

‘ Uzinduzi huu unakazia ahadi mpya ya Faidika isemayo Tuboreshe maisha’.ameongeza Dlamini. 

Faidika imefanikiwa kuwafikia zaidi ya watanzania 45,000 nchi nzima ambapo wmenufaika katika maswala ya kifedha kutoka na huduma hizo kutolewa kwa urahisi, stahiki na kwa unafuu zaidi.

Letshego ni taasisi inayotoa huduma za kifedha ambayo imejitolea kuendeleza ujuzi na vipaji na ina zaidi ya vituo vya uwakilishi 268 kupitia mitandao yake inayohudumia zaidi ya wakopaji laki tatu na wawekaji laki moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...