Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR
 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo amewaasa watanzania kuchukua tahadhari na watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwa kuwaaminisha wananchi kuwa maandamano na vurugu ndio demokkrasia na ukombozi wa umaskini wetu. 

Kanali Kondo alisema kuwa watu wa aina hiyo ni wakuogopwa kama ukoma kwani ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu ambapo tunashuhudia vurugu, vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali duniani na madhara yake. 

“watanzania tuchukue taadhari ya watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwani kumekuwa na watu wanaotuhamasisha ya kuwa maandamano na vurugu ndiyo ukombozi wa umaskini wetu hivyo tunapaswa kuchukua taadhari na kukataa hadaa hizo” alisema Kanali Kondo. 

Vilevile aliongeza kuwa, roho mbaya imechangia taifa letu kudumaa kimaendeleo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wetu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wasomi na wananchi wa kawaida. 

Aidha,alifafanua kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais John Pombe Magufuli amechukua hatua ngumu ya kupambana na vitendo vya rushwa, ubadhilifu na ufisadi kwani kitendo hicho kimewaudhi mafisadi na mawakala wanaopotosha ukweli na kuendesha propaganda chafu dhidi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2016

    The mdudu, Asante sana hilo tushaligundua watanzania hatu danganyiki ndio maana kila kukicha magazeti mengi huandika mabaya kuliko mazuri ila wengi wetu tu nayaona mabadiliko ya ukweli yakifanyika kwa vitendo tena kwa kasi ya hali ya juu hayo MADAWATI ya shule ni mojawapo ya mabadiliko ya ukweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...