Huu ni Muendelezo wa Matukio Madogo Madogo yanayo endelea Kujitokeza katika eneo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya ambapo ndipo Sehemu pekee kati ya Sehemu zote kwa Jiji zima kuwekwa Taa za kuongozea Magari na watembea kwa Miguu kwa Mkoa mzima wa Mbeya kiukweli hapa ndipo ambapo pamepewe kipaumbele hicho cha kuwekewa Taa za kuongozea Magari na Watembea kwa Miguu, Lakini cha kushangaza zaidi licha ya eneo hilo kupewe kipaombelele kumekuwa na Vijipu Upele vingi ambavyo vinajitokeza mara kwa mara katika eneo hilo ikiwemo hili la Taa moja Kupigwa Ngwala na Gari na kutelekezwa kama uionavyo hapo katika Taswira ikiwa na Mmoja wa watembea kwa Miguu akisubiri Taa hiyo iweze kumuongoza lakini hali ya kuwa Taa hiyo ikiwa hoi Bin Taabani kutokana na kupokea Ngwala na Gari ambayo hatukuweza Kuifahamu.
Kichwa cha Taa hiyo Mpya iliyo wekwa hivi karibuni kuajili ya kuongozea Wananchi watumiao Barabara hiyo ikiwa katika Uso wa simanzi Kando kando ya Eneo hilo la Mafiati Mataa Jijini Mbeya..
Mmoja kati ya watumiaji wa Barabara hiyo akisubiri Msaada wa Mbinu nyengine ya kumuwezesha kuvuka Barabara kutokana na kumsubiri Muongozaji wake alie Pigwa Ngwala bila mafanikio.
PICHA NA MR.PENGO MMG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2016

    Trafiki wako wapi?, na hiyo ni kazi yao ya kwanza. Kuhakikisha watembea kwa mguu na vivuko vyao wako salama.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2016

    Huwa nasikutishwa sana tena sana jinsi madereva wazembe wanavyo gonga alama za usalama barabarani bila kuchukuliwa hatua. Napendekeza faini iwe kubwa mno. Dereva yeyote akigonga taa za barabarani au alama yoyote..atozwe faini kubwa. Hii kazi wapatieni wananchi. Gari ikigonga mtu yeyote atakaye toa taarifa apewe zawadi kama motisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...