Kiwanda cha kutengeneza vyuma cha MMI Steel kilichopo katika eneo la viwanda mikocheni
jijini Dar es Salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni kumi na kutakiwa kulipa faini hiyo baada
ya siku saba kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira na kanuni zake ya mwaka 2004, kwa
kutiririsha maji machafu katika maeneo ya mtaa wa TPDC kwa warioba jijini dar es salaa. Maji
ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.
Adhabu hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea eneo la mtaa wa viwanda mikocheni kufuatia uchafuzi wa
mazingira unaotokanao na utitiririshaji wa majitaka katika maeneo hayo.
Wakati huohuo, Shirika la maji safi na majita taka Jijini Dar es Salaam na Pwani ( Dawasco)
limepewa siku kumi na saba kumaliza tatizo la utiririshaji wa maji taka katika mtaa wa TPDC
mikocheni kwa Warioba jijini Dar es Salaam.
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri Mpina Baada ya kufanya usafi jumamosi ya mwisho
wa mwezi wa tatu na kutoa siku saba kwa DAWASCO na NEMC kusimamia suala zima la usafi
wa mazingira na agizo lake kuupuzwa.
Awali, Mhe. Mpina alisema kuwa uchafuzi wa mazingira hauwezi kuendelea kuvumiliwa na
lazima hatua za kisheria zichukuliwe, na kuwaasa watendaji wa taasisi za serikali kuyapa
kipaumbele maagizo yanayotolewa na viongozi wa ngazi za juu za serikali kinyume na hapo ni
kutokutii mamlaka. “tasisi za serikali lazima zifanye kazi kwa kushirikiana kutokana na kwamba
kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NEMC, dawasco na Manispaa ya kinondoni katika suala
zima la utatuzi wa uchafuzi wa mazingira katika mtaa wa TPDC.” Alisema.
Naibu waziri Mpina aliongeza kuwa ifikapo tarehe 30/7/2016 asikutane tena na tatizo la
uchafu na harufu mbaya katika mtaa wa TPDC kwani hali hiyo ni hatari sana kwa afya ya wakazi
wa maeneo hayo na mazingira.
Kwa upande wake DAWASCO ikiwakilishwa na Injinia Erick Jackson alisema kuwa Tangu
muheshimiwa Naibu Waziri Mpina atoe agizo la uondoshwaji wa majitaka na uboreshwaji wa
miundombinu katika mtaa huo, wamekuwa wakifanya kazi na bado inaendelea na kazi hiyo
pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kifedha na ufundi.
Hata hivyo uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya kinondoni umelishitaki shirika la maji safi na
maji taka jijini dar es salaam na Pwani DAWASCO ,kiwanda cha MMI steel na Tembo Tiles kwa
uchafusi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka.NA EVELYN MKOKOI
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akisikiliza
maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa wa (TPDC)Bw, Idrisa Hashimu kuhusu Uchafuzi wa
Mazingira Unaofanywa na viwanda katika mtaa huo.
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa
katika ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha MMI steel kinachotuhumiwa Kuchafua mazingira katika
mtaa wa TPDC.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...