Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, liitwalo Asvoko, limeiomba serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashataka mwanamuziki Koffi Olomide. 

Hii ni baada ya kuonekana katika video iliyosambaa mitandaoni akimpiga teke mmoja wanamuziki wake wa kike kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi ijumaa wiki iliopita.

Wakati huo huo shirika la Zambia la kilimo na biashara limefutilia mbali tamasha ambalo Koffi alipanga kulifanya nchini humo lililokuwa linatarajiwa kufanyika kuanzia Jumatano hadi Jumatatu Ijayo. Raisi wa taasisi hiyo Ben Shoko amesema kitendo hicho alichokifanya mwanamuziki huyo wa kimataifa katika muziki wa dansi sio cha kiungwana kabisa.

Ijumaa iliyopita katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata JKIA Nairobi Koffi alinaswa katika video akimpiga teke dansa wake huyo kwa kilichodaiwa alikorofishana na mwanamuziki wa kundi hilo aitwaye Cindy Le Couer ambaye amekuwa na mahusiano naye wa kimapenzi toka 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...