Meneja Mwakilishi wa Kupatana.Com, Makusaro Tesha akizungumza na waandishi wa habari juu huduma mpya ya Premium waliyoizindua katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu JK. Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo Mabango ya Huduma za Premium, Gift Joshua huduma mpya ya Premium waliyoizindua katika maonesho ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu JK. Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
TANZANIA ni nchi inayokuwa katika teknolojia ya mawasiliano katika kurahisha kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya biashara ya kimataifa yanayofanyika katika viwanja v ya Mwalimu Julius Kambarage nyerere, Meneja Mwakilishi wa Kupatana.Com, Makusaro Tesha amesema na kongezea kuwa wananchi wanaweza kutangaza biashara katika kutumia mtandao. Amesema Kupatana.com imeanzisha huduma ambayo Premium ambayo kwa wale watu wanaotaka kutangaza biashara kwa haraka na kuweza kupata wateja mara moja.
Makusaro amesema Kupatana .com ni mtandao wenye soko kubwa nchini kwa kuendesha huduma za kimtandao kwa wananchi kuendesha biashara mbalimbali ya yenye watu milioni 24.7 wanaotembelea.
Amesema kuwa mauzo yanayofanywa katika mtandao huo kwa siku ni zaidi ya vitu 80,000 hali hiyo inaonyesha watanzania wanakwenda na teknolojia.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...