Mkurugenzi wa Benki ya Azania Godfrey Dimoso akizungumza katika hafla ya futari waliyowaandalia Masheikh na wadau mbalimbalu wa kampuni hiyo na kuwataka kufuata nasaha zilozotolewa na masheikh hao.
Baadhi ya wadau wakifuturu.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHEIKH Mahamoud Abdallah Waziri amewataka waislamu kuweza kujikita kwenye fungamano la Amani ambalo huwakutanisha watu kwa pamoja na kuwasihi kudumisha utamaduni huo ili kuendeleza amani ambayo ni tunu ya Taifa letu. Amesema hayo wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya Azania ambapo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Sheikh Waziri amewasa jamii kujikita zaidi kwenye fungamano la Amani
na kuwataka watanzania kudumisha utamaduni wa kujumuika pamoja, kufurahika au kubadilisha mawazo ili kuendeleza amani ambayo ndiyo tunu ya Taifa letu.
Ameweza kuupongeza uongozi wa benki hiyo kwa kufanya tukio hilo adhimu la kuwakutanisha wadau mbali mbali, hasa katika kumi la mwisho la Mwezi mtukufu la Ramadhani ambalo ni kumi la Fiedaus lenye maana ya kuomba pepo kwa Mwenyezi Mungu.
Naye Sheikh Muhammed Idd 'Abu Idd', amesema Saumu ni mchango ambao una malengo kwa anayefunga kuendelea na kuwa mtu mwema hata baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani."Moja ya malengo au hekima ya Saumu ni kumfanya mtu aishi vema na jamii yake na kwamba Mwezi huo umeletwa ili kuwabdili watu kutoka kwenye uasi kwenda kwenye wema," amesema. Ameongeza na kusema kuwa lengo lingine la saumu ni kutengeneza afya kwa wafungaji jambo ambalo hata matabibu wamekuwa wakilisisitiza.
Naye Mkurugenzi wa Benki ya Azania, amewapongeza wateja na wadau wao kwa kukubali wito wao na kuhudhiria tukio hilo ambalo anaamini wamepata vitu vya ziada kutoka kwa Masheikh waliotoa nasaha. Amesisitiza kuwa benki hiyo ambayo ni wazawa kwa asilimia 100 itaendelea kuwahudumia watanzania katika mahitaji yao wanayohitaji.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...