Mahakama
ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma juu ya habari
iliyoandikwa na gazeti la kila siku la Mwananchi toleo la Jumanne, Julai
12, 2016. Gazeti hilo lilichapisha habari ambayo Mwandishi wa habari
hiyo alimnukuu Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Katarina
Revokati akiwataka watendaji wa mahakama nchini kujenga utamaduni wa
kuwajibika na kutoruhusu uhuru wa mahakama kuingiliwa na watu kutoka nje
ya Mahakama.
Kutokana na habari hiyo, Mahakama ya Tanzania inakanusha taarifa hiyo kwa kuwa ililenga katika kuipotosha jamii na kuleta msuguano kati ya Mahakama na Taasisi nyingine.
UFAFANUZI WA TAARIFA HIYO
Mahakama ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi wa alichokisema Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano kuhusu Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania Jumatatu Julai 11, 2016 mjini Dodoma.
Aidha, Msajili aliwataka watumishi wa mahakama nchini kutekeleza mpango mkakati kwa nia thabiti na siyo kuutumia uhuru wa mahakama vibaya kufunika maovu, badala yake aliwataka wale wenye kasoro katika utendaji wa kazi kujirekebisha wao wenyewe ndani ya mahakama la sivyo watarekebishwa hata kutokea nje kwani jamii yetu kwa sasa imedhamiria kubadilika na haitavumilia utendaji mbovu kwa kigezo cha uhuru wa mahakama.
Mahakama ya Tanzania inapenda kuujulisha umma kuwa inafanya kazi na watu wote na wadau wote nchini ili kuhakikisha nchi inaenda inavyotakiwa na haitaogopa kukosolewa kinyume na picha iliyopelekwa kwa jamii na habari iliyopotoshwa kwenye gazeti la Mwananchi.
Mahakama inashauri waandishi wa habari kuwasiliana na Mahakama endapo kuna jambo lolote linalohitaji ufafanuzi. Makosa mengine katika taarifa ni kama vile kukosea cheo kwa kusema Jaji badala ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na kuandika taarifa kuhusu hatua zinazochuliwa kwa Wahe. Majaji waliohusika na sakata la ESCEOW ambapo kiukweli katika mkutano huu halikuongelewa kabisa.
IMETOLEWA NA KI TENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...