Na Bashir Yakub.

1.WARRANTY NININI KATIKA BIASHARA.

Warranty ni mkataba kati ya mtengeneza bidhaa na mnunua bidhaa ambaye naye anakwenda kumuuzia mtu wa tatu( mteja). Kunakuwa na watu watatu. Kwanza ni mtengeneza bidhaa, pili ni mnunua bidhaa ambaye naye anakwenda kuuza(mfanyabiashara) na tatu ni mnunua bidhaa (mteja) anayenunua kwa ajili ya matumizi.

Kwa mfano una duka la simu kariakoo, we ni mfanyabiashara. Yule aliyekuuzia simu kwa mfano tecno company huyo ni mtengenezaji. Na anayekuja kariakoo kununua simu kwa ajili ya matumizi huyo ni mteja. Kwahiyo kisheria Warranty ni mkataba kwa ajili ya hawa watatu katika kuhakikisha ubora na ufanisi wa bidhaa.

2. JE MIMI KAMA MFANYABIASHARA NINALAZIMIKA KUANDIKIWA MKATABA WA WARRANTY .

Ndio unaponunua bidhaa popote kwa ajili ya kuuza tena ni lazima uwepo mkataba wa warranty . Ni mkataba wa warranty pekee utakaokuweka salama na bidhaa uliyonunua. Mfanyabiashara sio mtengeneza bidhaa na hivyo kwake sio rahisi kujua ubora, muda wa kuishi wa bidhaa,pamoja na mambo mengine yanayohusu uimara na ufanisi wa bidhaa katika matumizi.

Ni kutokana na hilo analazimika kupata mkataba wa warranty ambao ndio uhakiki na ithibati ya ufanisi na ubora wa bidhaa.

3. JE KUNA TOFAUTI KATI MKATABA WA KUNUNUA BIDHAA NA MKATABA WA WARRANTY.

Ndio kuna tofauti. Mkataba wa kununua bidhaa ni mkataba wa kununua kama neno lilivyo na hueleza kuhusu manunuzi. Wakati mkataba wa warranty ni mkataba ambao hauelezi jambo jingine lolote isipokuwa ubora katika matumizi ya bidhaa, ufanisi wake, muda wa matumizi, na kila jambo linalohusu uimara na umathubuti wa bidhaa.

Pia lazima ueleze nini kitatokea iwapo bidhaa haitafanana na maelezo hayo. Ikiwa bidhaa itarejeshwa, au pesa ya manunuzi itarejeshwa au vinginevyo, ni lazima ielezwe. Hii ndio huitwa “warranty contract.”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...