Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Mradi wa Jukwaa la Kijani la wanawake Nchini wahakikishe wanaendelea na mkakati wa kuelemisha wanawake kuhusu namna ya kukukabiliana na mabadiliko ya Tabia hapa Nchi.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati anazindua mradi wa GREEN VOICES,mradi unaolenga kusaidia wanawake kukabiliana na mabadiliko ya Tabia,unaofadhiliwa na Rais wa Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Maria Tereza Fernandes De la Vega .

Makamu wa Rais pamoja na kupongeza jitihada zinazofanywa na Jukwaa hilo katika kusaidia wanawake kupambana na mabadiliko ya Tabia ya nchini, amesema bado upo umuhimu mkubwa kwa wanawake kuelimishwa zaidi kuhusu mabadiliko hayo kwa sababu wao ni moja ya kundi ambalo linaguswa na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo suala la ukame.

Amesema bara la Afrika linapoteza mabilioni ya dola kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi ikiwemo tatizo la ukame ambao umechangia kupunguza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa kiasi kikubwa pamoja na uhaba wa maji.

Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema nchi za Afrika bado zinakabiliana uhaba wa kifedha,taarifa sahihi na teknolojia katika jitihada za kupambana ipasavyo na mabadiliko ya tabia ya nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Green Voices Tanzania uliofanyika katika hoeteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo namna ya mkaa wa karatasi unavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mchau Windmill Ndugu Laurian Mchau wakati wa uzinduzi wa mradi wa Green Voices Tanzania .
Keki ya Muhogo.
Mkaa wa karatasi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassanakipata maelekezo ya namna zao la muhogo linavyoweza kuwa na idadi nyingi ya vyakula.
Mshauri na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Mhe. Getrude Mongella akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Green Voices Tanzania uliozindiliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...