Mlimbwende (miss) Mbeya 2016 Eunice Robert amewatembelea watoto yatima katika kituo cha Amani Nsalaga Uyole mkoani Mbeya hivi kalibuni na kuchangia baadhi ya mahitaji katika kituo hicho ikiwemo mchele, unga, sabuni, mafuta yakupikia, nguo, Daftari, Kalamu na Mafuta yakupaka. Aidha Mlimbwende huyo kutoka chuo kikuu cha Teofilo Kisanji ambaye ndiye anayeshikiria Taji la Umiss kwa sasa kwa Mkoa wa Mbeya amewaomba watu Binafsi, Mashirika ya Kidini, na Viongozi Mbalimbali wawe na mazoea ya kuwatembelea watoto yatima, Wazee, Watu wasio jiweza, Wagonjwa na wale waliopo katika Mazingira magumu na kuwasaidia kwa kuwa Jamii hiyo inahitaji Msaada kwa kiasi kikubwa hivyo sote tuguswe na hili.
PICHA NA ECKY THE BEST MMG MBEYA. Miss Mbeya 2016 Eunice Robert akiwa na baadhi ya Watoto kutoka katika Kituo cha kulelea Watoto Yatima Amani kilichopo eneo la Nsalaga Jijini Mbeya.Pia Miss Mbeya akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Michezo mbalimbali na watoto wa Amani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...