MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Wakili Jumaa Mhina 'Pijei', baada ya kula kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam juzi, amesema kazi kubwa iliyo mbele yake ni kuhakikisha anatatua kero mbalimbali za wananchi wa wilaya hiyo.
Akizungumza
katika viwanja vya Ikulu baada ya kula kiapo, Pijei, akiwa na
wakurugenzi wenzake, alisema kuwa, kwa kushirikiana na viongozi wenzake
wa wilaya hiyo akiwemo Mkuu wa wilaya, Daniel Chongolo na Ofisa Tawala
wa wilaya watatekeleza majukumu yao ipasavyo.
"Ninaamini
kwa kushirikiana na viongozi wenzangu walioteuliwa hivi karibuni,
tutajitahidi kutatua kero za wananchi wetu," alisema.
Pijei alisema kuwa, uamuzi wa Rais John Magufuli kumteua kuwa mkurugenzi
wa wilaya hiyo, umempe nguvu na kujiamini kuwa, hatamwangusha Rais
Magufuli na wakazi wa wilaya hiyo.
Alisema
licha ya wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto nyingi atahakikisha
wanatumia fursa mbalimbali kutatua kero hizo wakati wowote.
Wakili huyo alisema kuwa, pia atashirikiana na wenzake kuhakikisha
wanaibua miradi mbalimbali itakayowainua kimapato vijana na akina mama
wa wilaya hiyo.
"Hii wilaya iko mpakani na Kenya, hivyo tutatumia fursa zilizopo kwa kushirikiana na wananchi kuanzisha miradi itakayowainua kiuchumi, naamini Longido ina wananchi waelewa na wapenda maendeleo," alisema.

mara baada ya kuripo katika kituo chake cha kazi, atapata sehemu ya
kuanzia kwani atakuwa amepata ripoti kamili ya wilaya hiyo na hata
kutembelea sehemu mbalimbali.
Wakili Jumaa Mhina 'Pijei' (wa kwanza kulia mbele), akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakili Jumaa Mhina 'Pijei' (wa kwanza kulia), akisaini kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...