Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akiyekaa, akimuonyesha
Mwanachama huyu wa Mfuko huo michango yake papo kwa hapo kwenye banda
la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa
maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Julai 4,
2016. Mamia ya Wananchi wamekuwa wakimiminika kwenye banda hilo, ambapo
jambp la kuvutia Mkurugenzi Mkuu huyo aliungana na wafanyakazi wake
kutoa huduma kwa wananchi. Maonyesho hayo yanashirikisha jumla ya nchi
30 ambapo banda la PSPF limekuwa na idadi kubwa ya wananchi
wanaotembelea kujua huduma zitolewazo kwa wananchi ambao si wanachama
lakini pia kuwahudumia wanachama wake. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)

Mama
Anna Mkapa, (kulia), Mke wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye ni
Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa Kwa Wote (EOTF), akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto) na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati Mkurugenzi huyo
alipotembelea banda la EOTF linalokusanya wajasiriamali kutoka mikoa
yote ya bara na vuisiwani. Kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari yaani
PSS, wajasiriamali hao wanaweza kujiunga na Mfuko huo na hivyo kufaidika
na mafao mbalimbali yakiwemo ya kuboresha biashara zao
Mama
Salma Kikwete, (kulia), Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete,
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, walipokutana
kwenye banda la EOTF kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam, Julai 4, 2016.
Mamia ya wananchi wakiwa kwenye banda la PSPF Julai 4, 2016
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akimkabidhi kadi yake ya uanachama wa Mfuko huo, Mwanaidi Msangi baada ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), Julai 4, 2016.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...