Mkuu mpya wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilayani humo leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Ofisi. Katika hafla hiyo, Taraba aliwataka watendaji wa wilaya hiyo kujituma kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano pamoja na kuwa waadilifu katika kuwatumika wananchi. Aidha, alimpongeza Mkuu wa wilaya hiyo aliyestaafu, Hawa Ngh’umbi kwa utendaji wake huku akiahidi kuendelea kuchota hekima zake.
Mkuu wa Wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo wakati akiagwa baada ya kustaafu.
Mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake, Hawa Ngh’umbi (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mkuu mrithi wake, Nyabaganga Taraba wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo. Wengine kuanzia kushoto waliokaa ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kangese, Mkuu wa wilaya mstaafu, Hawa Ngh’umbi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo, Wilson Nyamunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...