MWALIMU HOUSE-NAFASI ZA UPANGAJI.
Kampuni ya Walimu ya (Teachers’ Development Company Limited) inayo furaha kuutangazia umma nafasi za upangaji katika jengo la MWALIMU HOUSE lililopo Kiwanja Namba 48 Kitalu ‘Y’, ILALA BOMA jijini Dar es Salaam. Jengo linapakana na Barabara ya Uhuru na Kawawa mkabala na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Soko la Karume na Ilala maarufu kama Ilala Boma.
Nafasi zilizopo katika jengo zinaweza kutumiwa kwa shughuli mbalimbali za kiofisi, maduka, bank, zahanati, mgahawa, chuo nk.
Nafasi za upangaji zinapatikana kuanzia ghorofa ya kwanza hadi ya nane kwa ukubwa wa kuanzia square mita 42 hadi 218. Gharama ya Upangaji ni Tshs. 24,000 (Bila VAT) kwa square mita moja ikijumuisha kodi ya pango (rent) na baadhi ya huduma zinazotolewa katika jengo (service charge).
Huduma zifuatazo zinatolewa katika jengo letu la Mwalimu House;-
(i) Genereta (Stand by Generator) (Mpangaji atachangia fedha kidogo ya mafuta ya Generator)
(ii) Tenki kubwa la kuhifadhi Maji
(iii) Lifti ya kubeba watu 10 kuanzia ghorofa ya chini (Basement) hadi ya nane.
(iv) Eneo kubwa la Parking (Inalipiwa)
(v) Usafi na Ulinzi (Masaa 24)
Gharama nyinginezo zitakazolipiwa na mpangaji ni kama ifuatavyo-;
Tozo ya kuandaa nyaraka mbalimbali (Documentation fee)-Tshs. 236,000/-Italipiwa mara moja katika kipindi chote cha upangaji.
Tozo ya bima ya pango (security Deposity)-ni kodi ya mwezi mmoja- Italipiwa mara moja katika kipindi chote cha upangaji -Itarudishwa endapo mpangaji atahama bila kufanya uharibifu katika eneo la upangaji.
Kwa maelezo zaidi au kuona maeneo yanayopangishwa, Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupitia:-
Simu ya Mkononi: 0769 084939, 0713 495603, 0765 187365
Simu ya Mezani: 0222203063
Email: tdevcoltd@gmail.com;khadijagogo@gmail.com.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...